Masila. Makau

Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS? Part 2

VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.

 

  1. RIBA

Riba ya mkopo katika VICOBA ni ndogo (mara nyingi haizidi 10%) sababu ya dhamira yake na pia aina ya wanachama waliyomo ndani ya vikundi lakini riba kwenye saccos huwa ni kubwa zaidi lakini Riba katika SACCOS ni kubwa maana hata mikopo yao ni mikubwa pia (mfano mikopo ya viwanja, mashamba)

 

  1. GHARAMA ZA UENDESHAJI

Gharama za uendeshaji wa VICOBA ni ndogo kwani hakuna ofisi (wanachama huchagua mahali pa kukutana kwa muda usiozidi saa moja), vile vile viongozi wa VICOBA hawaajiriwi (wanafanya kazi za kujitolea) lakini kuwa SACCOS inahitaji gharama kubwa za uendeshaji kama kuwa na ofisi, kuajiri watu, gharama za usaijili n.k

 

Nb: Vikoba ikikua huweza kuunda Saccos